X posted from the swahili forum http://www.yahoogroups.com/group/kiswahili
the gentleman below is a Kiswahili professor in Germany
Chifu
Group Moderator
Re: [Kiswahili] We have no Tribes in Kenya/on Waswahili another reply
Wenzangu,
Assalaamu alaykum.
Mimi sitaki kuuingilia mjadala huu kwa sababu haya ni maji makuu nami;
na maji yangu mimi ni ya magotini. Naogopa nisije nikazama! Hata
hivyo, najifunza mengi kutokana na yazungumzwayo hapa kuhusu mada hii.
Nitakalo kuongeza ni kusaidia kuikidhi haja ya Bwana Maur Abdalla
Bwanamaka kuhusu mbari. Hizi zifuatazo ndizo mbari za Waswahili wa
Pwani ya Kenya nilizozipata:
1. MBARI ZA WAKILINDINI
Mbari ya Mwinyi Nguti wa Mwinyi Mwenzagu
" Mwinyi Humzi
" Mwinyi Kombo wa Dani
" Mwinyi Kae wa Pembe
" Mwinyi Hudumzi
(Kama sikukosea, nafikiri mbari ya Bwana Stambuli ni hiyo ya Mwinyi
Nguti wa Mwinyi Mwenzagu).
2. MBARI ZA WATANGANA
Mbari ya Mwinyi Muli
" Mwinyi Mjaka
" Mwinyi Umbwi
" Mwinyi Ngwisa
3. MBARI ZA WACHANGAMWE
Mbari ya Mwinyi Kitue
" Mwinyi Mgosi
" Mwinyi Mfaki
" Mwinyi Koba
" Mwinyi Ngovo
4. MBARI ZA WAMVITA
Mbari ya Mwinyi Kutani
" Mwinyi Kae
" Mwinyi Hunziali
5. MBARI ZA WAMALINDI
Mbari ya Banu Shasha
" Banu Mbwana
6. MBARI ZA WAJOMVU (au WAJUNDA)
Mbari ya Mwinyi Faki
" Mwinyi Chande wa Shamaniya
" Mwinyi Usi Muhija
" Mwinyi Uledi wa Ndau
" Mwinyi Jaa wa Mwinyi Nguti
7. MBARI ZA WAMTWAPA
Mbari ya Mwinyi Nyali (au Mbari ya Ng'ombeni)
" Mwinyi Jimve
" Mwinyi Goziadi
" Mwinyi Rakwe
" Banu Muyaka
" Banu Shemapwe
8. MBARI ZA WAKILIFI
Mbari ya Mwinyi Shoka
" Mwinyi Kiwanda
" Mwinyi Mkomati
" Mwinyi Gome
9. MBARI ZA WAPATE
Mbari ya Wa-Pate
" Wa-Amu
" Wa-Kitau
" Wa-Twaka
" Wa-Tukut
" Wa-Kipungani
" Wa-Barawa
" Wa-Shela
10. MBARI ZA WAGUNYA (au WABAJUNI)
Mbari ya Washaka
" Wa-Uziwa
" Wa-Ungama
" Wa-Ozi
" Wa-Sada
TANBIHI: Mimi ni mjumbe tu; basi nisiuwawe!! Nimezipata mbari hizi
kutoka kurasa 49-50 za kitabu kiitwacho Life and Politics in Mombasa,
kilichoandikwa na Hyder Kindy, na kuchapishwa na East African
Publishing House, Nairobi, 1972.
Wassalaamu alaykum.
Mwenzenu,
Abdilatif Abdalla
--
TO ADVERTISE HERE, SEND KSH 500 to +254 726 034 530
NEXT SOCIAL MEETUP http://on.fb.me/dafJDE
TECHMTAA BLOG: http://www.techmtaa.com/
To unsubscribe from this group, Email mlalahoi+unsubscribe@googlegroups.com
Websites for Ksh 10,000? Email robertnng@gmail.com
No comments:
Post a Comment